Maandalizi ya sherehe ya kuhitimu tarehe 5/9/2015, ambayo itafanyika sambamba na anniversary ya miaaka mitano ya chuo hapa karagwe yanaendelea huku washiriki wakishauriwa kutuma michango yao mapema ili kuwezeza bajeti vizuri. kila mhitimu atatakiwa kulipia Tsh.40,000 zikiwa ni ada ya majoho 12,000, ada ya chakula 10,000, ada ya mziki, mapambo 15,000 na ada ya ukumbi 3000. kila mhitimu atapewa kadi mbili (yake yeye na ya mzazi/ mlezi wake, kwa gharama hizihizi). wageni waalikwa pamoja na wanachuo wengine watachangia single coupon 10,000, double 15,000. mwisho wa kuwakilisha mchango ni tarehe 28/08/2015. njoo tusherekee pamoja na pia tuwajue waliosoma DAPA COLLEGE. Ikumbukwe kua sherehe hii ni lazima kwa kila mhitimu, na wote ambao bado hawajachukua vyeti vyao wanatakiwa kufika ili kupokea vyeti hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni